Habari ambazo zimeanza kuenea mitandaoni kuanzia asubuhi ya jumatatu ya leo ni kuhusu Aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha Wananchi CUF Pro Ibrahim Lipumba akihusishwa kujiunga na chama cha ACT WAZALENDO.
Habari hiozo zimechagizwa zaidi na Baadhi ya maafisa wa ACT WAZALENDO kutumia mitandao ya kijamii kumnadi kwa kasi Mwenyekiti huyo wa zamani wa CUF aliyejiondoa mwenyewe.
Moja ya maafisa wa kitengo cha mawasiliano wa ACT WAZALENDO ameonekana akitumia mitandao kutuma baadhi ya post za kumuonyesha LIPUMBA akiwa na ZITTO huku akiandika maneno ambayo yamekuwa yakiibua midadala kwa watanzania.
ZITTO KABWE amekanusha hakuna mwanachama mpya anayejiunga na chama hicho na wala hakuna ajenda kama hiyo inayojadiliwa ndani ya kikao hicho.
2/2 hatuna mjadala kuhusu wanachama wapya.Mkumbuke tu hao wanaoeneza tuna wanachama wapya ndio hao hao walisema hivyo hivyo 2015. Ikawaje?
Labda kuna kikao kingine kujadili Hilo. Sio hiki nilichomo Mimi sasa hivi
![]() |
Wataalam wa siasa wanasema ni muda wa kusubiri na kuona Je nini Kitajiri na kujua Ukweli na uongo wa jambo hili





0 comments :
Post a Comment