Wapo watu wengi sana ambao si wanamazoezi au wanamichezo na hawajapata fursa au muda stahiki wa kufanya mazoezi ya nguvu na wanahitaji kufanya mazoezi kwa ajili ya kuiweka miili yao vizuri na kuimarisha afya zao na pia wapate muonekano mzuri wanapovaa nguo zao.
Lakini wanakutana na changamoto mbalimbali za kimaisha zinazowafanya washindwe kutenga muda mrefu zaidi katika kufanya mazoezi, hata hivyo si lazima mtu apoteze muda mrefu akifanya mazoezi ili apate mabadiliko chanya katika mwili wake, zipo njia mbadala na rahisi ambazo mtu huweza kuzitumia ili kufikia malengo anayoyaazimia.
Yafuatayo ni mazoezi marahisi ambayo mtu huweza kuyafanya kila siku na akapata mabadiliko chanya katika mwili, mazoezi haya yana tija nyingi ambazo mtu akiyafanya kiufasaha zaidi huweza kupata mabadiliko ya haraka katika mwili wake .
Azimio kubwa la hili andiko ni suala la mazoezi na orodha ya mazoezi hapo chini itamsadia mtu kupata mabadiliko ya kimwili kulinganana tofauti ya kibayolojia na kimazingira ya mtu mwenyewe.

1.Kutembea
Kutembea ni suala rahisi mno lakini ni kitendo chenye nguvu na tija mwilini, kutembea husaidia kupunguza kiwango cha cholesterol mwilini, kukomaza mifupa, kuweka mapigo ya moyo sawa, kuleta uchangamfu, kushusha chini hatari na uwezekani wa kupata magonjwa mbalimbali kama kisukari na ugonjwa wa moyo. Kitendo cha kutembea kwa dakika 60 kwa siku ni zoezi tosha kwa mwili kwa bindamu.

2.Kuogelea
Kwa lugha rahisi kuogelea huitwa zoezi kamili, maji husaidia kunyoosha viungo ambavyo vimelegea na vina maumivu kutokana na kutofanya mazoezi kwa muda mrefu, tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa kuogelea kunaboresha hali ya akili na kumfanya mtu awe katika hali ya uchangamfu. Na kupunguza kalori mwilini.

3.Squats
Zoezi hili ni zuri katika kupunguza kalori mwilini kwasababu linahusisha misuli mingi zaidi katika ufanyaji wake. Zoezi hili hufanywa kwa mfumo wa kuchuchumaa ama kukaa na kusimama kwa awamu na mizunguko mingi (reps).

4.Push –ups ( pushapu)
Dhamira kuu la hili zoezi ni kukaza mwili eneo la juu, kati na chini kwa wakati mmoja, mtu huweza piga push up 15 hadi 20 kwa wakati mmoja.

5.Kukimbia
Mtu uweza kukimbia kwa dakika 30 au 45 ama zaidi mfululizo bila kusimama kwa kasi tofauti, kukimbia huchangamsha akili, mwili na husaidia kupunguza mafuta mwilini pamoja na kukomaza misuli na mifupa mwilini.

6.Inama – inuka (bent-over row)
Zoezi hili huonekana rahisi kutokana na jina lake na mazoea ya watu kuinama na kuinuka katika vitendo ama kazi mbalimbali za kila siku lakini mtu anapofanya mara nyingi kwa wakati mmoja huwa zoezi tosha la kuuweka mgongo, miguu, tumbo na shingo katika hali nzuri ya kujinyoosha.



0 comments :
Post a Comment