Jumatatu ya Septemba, 5 katika mitandao mbalimbali zilisambaa habari ambazo zinamhusisha aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba kujiunga na ACT-Wazalendo.
Kiongozi Mkuu wa ACT, Zitto Kabwe amejibu tetesi hizo na kusema kuwa jambo hilo halina ukweli na kama likitokea watatoa taarifa kwa umma.
“Fununu hizo sio za kweli, chama chetu kipo wazi mtu yoyote ana haki ya kujiunga iwapo atakuwa anakubaliana na misingi ya chama, tuna misingi 10, katiba ya chama na itikadi ya chama,
“Mtu yoyote raia wa Tanzania ambaye anajiona ni mzalendo ana uhuru wa kujiunga na chama chetu na pale ambapo jambo hilo litatokea tutawajulisha, chama chetu sisi ni cha uwazi,” alisema Zitto.
Zaidi waweza mwangalia kupitia video hapo chini.