Nahodha wa zamani wa Barcelona, Xavi Hernandez ametoa maoni yake kuhusu uwezo ambao anaonyesha winga wa mabingwa wa EPL 2015/2016, Leicester City, Riyad Mahrez.
Xavi ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Al Sadd ya Qatar alisema kuwa uwezo wa Mahrez kwa sasa anafaa kabisa kukipiga klabu yake ya zamani ya Barcelona.
“Mahrez ana uwezo wa kucheza Barcelona, lakini namfurahia kuchagua kusalia Leicester,
“Alikuwa na uwezo wa kufanya maamuzi, lakini Leicester wangekuwa wamepoteza mchezaji muhimu baada ya kupata mafanikio makubwa na ingekuwa aibu. Inapendeza kumwona akiwa na Leicester katika michuano ya Ulaya msimu huu,” alisema Xavi.