ALICHOKISEMA PLUIJM BAADA YA KUPATA TAARIFA ZA KUTIMULIWA YANGA..!!!


Kocha mkuu wa klabu bingwa Tanzania bara Young Africans, Hans van der Pluijm, amesema hahofii chochote kuhusu mabadiliko ya benchi la ufundi yanayozungumzwa na anaelekeza akili yake kuiandaa timu hiyo kwa ajili ya mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar .


Kesho jumatano Young Africans watakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar katika mfululizo wa ligi kuu Tanzania Bara, mchezo utakaopigwa uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam  ambapo Pluijm  alisisitiza kuhusu kufahamu umuhimu wa kushinda mchezo huo.

“Nimesoma kwenye magazeti jana na leo, lakini sijali hizo taarifa. Mwajiri wangu hajaniambia.

Na kuhusu mchezo wa kesho, Pluijm alisema awali alikuwa anajua ni Alhamisi, lakini jana ndiyo kaambiwa kwamba ni Jumatano.

Hata hivyo, Mholanzi huyo amesema hana namna nyingine zaidi ya kujiandaa kwa mchezo huo ambao ni muhimu kushinda ili kurejesha imani ya mashabiki katika mbio za kutetea ubingwa.

Habari za ndani kutoka Young Africans, zinaeleza kwamba benchi lote la ufundi litavunjwa na zitakuja sura mpya kabisa baada ya mzunguko wa kwanza wa ligi kuu.

Pluijm na wasaidizi wake, Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali na Meneja Hafidh Saleh wataondoka na Mzambia, George Lwandamina atakuwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na Boniface Mkwasa, Manyika Peter kocha wa makipa na Meneja, Sekilojo Chambua.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment