Hakuna Upendeleo Katika Kutoa Nafasi Za Ajira Za Idara Za Serekali za Jamhuri Ya Muungano


207

Na Masanja Mabula –Pemba

SEREKALI Ya Mapindunzi Ya Zanzibar Imesema Hakuna Upendeleo Katika Kutoa Nafasi Za Ajira Za Idara Za Serekali Ya Jamuhuri Ya Muungano Ikiwemo Jeshi La Wananchi Na Polisi Bali Zinatolewa Kulingana Na Sifa Ya Muombaji .
Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Makamo Wa Pili Wa Zanzibar Mh Mohammed Aboud Mnohammed Ameyasema Hayo Jana Alipokuwa Akijibu Suali Aliloulizwa Na Waandishi Wa Habari Kwenye Mkutano Wake Na Vyombo Vya Habari Uliofanyika Chake  Chake  Kisiwani Pemba.
Katika Suali Lake Mwandishi Wa Habari Sleiman Rashid Omar Alitaka Kujua Serekali Inachukua Hatua Gani Kuuondoa Upendeleo Katika Kutoa Ajira Kwa Idara Za Muungano Ambazo Wananchi Kisiwani Hapa Kwamba Nafasi Zinazoletwa Pemba Zinaporwa Na Kupewa Vijana Wanaotoka Unguja.
Waziri Aboud Alisema Serekali Ya Jamuhuri Ya Muungano Imekua Ikitoa Nafasi Za Ajira Katika Idara Zake Kwa Mikoa Yote Ya Zanzibar Ya Ulinzi Na Usalama Ya Kila Mkoa Kufikisha Majina Ya Vijana Ambaoni Wakaazi Wa Mkoa Huona Sio Vyenginevyo.
Alifahamisha Kwamba Ajira Zinazotangazwa Ni Chache Na Wanaojitokeza Kuomba Ni Wengi Hivyo Kunakuwako Na Uchambuzi Wa Kina Katika Kufanya Maamuzi Ya Kuchagua Vijana Wa Kujiunga Na Idara Hizo Kwa Kufikia Vielelezo Vya Kila Mmoja.
“Hakuna Upendeleo Nafasi Hutangazwa Na Wenye Sifa Huomba Lakini Ikumbukwe Kwamba Nafasi Ni Chache Na Wanaojitokeza Kuomba Ni Wengi Hivyo Kamati Hufanyakazi Ya Ziada Kufikia Kielelezo  Kabla Ya Kufanya Uteuzi Sioni Kwamba Kuna Upendeleo”Alifahamisha.
Aidhawaziri Aboud Alikiri Kuwepo Na Idadi Kubwa Ya Vijana Wasio Kuwa Na Ajira Ungujana Pemba Na Kufahamisha Kwamba Serekali Imeanza Kuchukua Hatua Za Maksudi Kuitafutia Ufumbuzi Changamoto Hiyo.
Alieleza Kuwa Miongoni Mwa Mikakati Hiyo Iliyoandaliwa Na Serekalina Ambayo  Imeanza Kutekelezwa Ni Kuahamasisha Wawekezaji Kuekeza Katika Sekta Ya Kilimo ,Uvuvi Na Utalii Ili  Vijana Waweze Kupata Ajira Na Kupunguza Ukali Wa Maisha Katika Familia Zao.
Aliongeza Kuwa Kupitishwa Kwa Sheria Mpya Ya Mafuta Na Gesi Itafungua Milango Kwa Wawekezaji Kuwekeza Mitaji Yao Na Hivyo Kutoa Fursa Kwa Vijana Kupata Ajira Pamoja Na Kupatikana Soko La Bidhaa La Wajasiriamali Wadogo  Wadogo.
“Kupitishwa Kwa Sheria Mpya Ya Mafuta Na Gesi Kutafungua Milango Ya Uwekezaji Pamoja Na Kuzalisha Ajira Kwa Vijana Na Kutanuka Soko La Bidhaa Za Wajasiriamali Wadogo Wadogo  Na Wakati “Alieleza.
Hivyo Alisisitiza Kuwa Serekali Imepanga Kuziendeleza Fursa Ambazo Bado Hazijatumika Kwa Maslahi Ya Taifa Kwa Kuziboresha Ili Zilete Tija Kwa Umma Na Taifa Kwa Ujumla.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment