Timu
12 zinatarajiwa kushiriki Ligi ya Taifa ya Wanawake inayotarajiwa
kuanza Novemba mosi, mwaka huu kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya
Maendeleo ya Soka la Wanawake na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), zilizoridhia tarehe hiyo.
Tayari
klabu zimeagizwa kuzingatia jina kuenenda na namba za jezi mgongoni ili
kuepusha mkanganyiko wa wachezaji wakati wa ligi hiyo inayofanyika kwa
mara ya kwanza nchini Tanzania.
Timu
12 zinatarajiwa kushiriki ligi hiyo ambako kesho Oktoba 8, 2016 itakuwa
ni siku ya kuchambua fomu za usajili wakati Oktoba 10, mwaka huu majina
ya usajili yatatangazwa ambako pia klabu zitatumiwa kupitia anwani za
barua pepe.
Oktoba
11 na 12, 2016 ni muda wa klabu kuleta mapingamizi yatakayosikilizwa
Oktoba 15, mwaka huu. Majina ya pingamizi yatatangazwa kabla ya Oktoba
20, 2016 na maandalizi ya ligi yataendelea.
Wakati
wote huo wa usajili, klabu hazina budi kutangaza aina ya rangi
wanazotumia katika michezo ya nyumbani na ugenini na kutakiwa kusafiri
na jozi zote mbili ili kuepuka mkanganyiko wa kufanana jezi.
Kutakuwa na jopo la makocha watakaofanya uteuzi wa wachezaji nyota watakaoitwa kwenye timu za taifa ambaye atagharamiwa na TFF.
Vyama
vya mikoa visadie klabu katika bajeti zao kwa vile tathamini inaonyesha
kuwa fedha zinazotoka hazitoshi. Vyama hivyo vya mikoa pia visaidie
maandalizi ya michezo kama vile kuandaa uwanja nakadhalika ukioandoa
waamuzi ambao watagharamiwa na TFF.
Hakutakuwa
na zawadi ya fedha zaidi ya kombe la medali kwa timu shiriki, labda
kama atatokea mdhamini mwingine. Hakutakuwa na zawadi kwa mchezaji bora,
mfungaji bora, kipa bora, ingawa kutakuwa na jopo la kuwachagua.
Mchezaji bora atachaguliwa kwenye hatua za mwisho wa mashindano,
mfungaji bora atachaguliwa kuanzia hatua ya kwanza ya mashindano.


0 comments :
Post a Comment