Baada
ya kumalizika mchezo wa VPL kwa Mbeya City kupata kichapo cha goli
mbili kwa bila kutoka kwa Simba, uongozi wa klabu hiyo umesema kuwa
umepokea matokeo hayo na kukubali kuwa wamefungwa kwa uwezo na Simba.
Hayo
yamesemwa na Msemaji wa Mbeya City, Dismas Temu na kusema kuwa ni hali
ya kawaida katika mchezo kupata matokeo mazuri au kupata matokeo mabaya
na hivyo wanakubaliana na matokeo kwani wapinzani wao walitumia vizuri
nafasi walizozipata.
“Ni
kawaida kupoteza mchezo, ni kawaida kufungwa ni kawaida kushinda huu ni
mchezo wa makosa, hatujajichanganya ni swala tu la mchezo wa soka, timu
yetu imecheza vizuri, swala la nafasi nani anatumia nani hatumii ni
jambo lingine,
“Simba
wametengeneza nafasi chache na wamefanikiwa kuzitumia, na sisi
tumetengeneza na tumeshindwa kuzitumia, hayo ndiyo matokeo na nadhani ni
jambo zuri kukubaliana na matokeo,” alisema Temu.


0 comments :
Post a Comment