KITENDO
cha jeshi la polisi kuwaweka ndani mahabusu zaidi ya saa 24 bila
kuwapeleka mahakamani au kuwapa dhamana ni ukiukwaji wa sheria na
uvunjifu wa ,katiba ya nchi.
Hayo
yalisemwana leo Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya
Katiba na Sheria, Mohamed Mchengerwa alipokuwa akifungua kongamano la
siku mbili la kitaifa la msaada wa kisheria kutoka mikoa yote ya
Tanzania bara na visiwani.
“Ni
kinyume cha sheria kuweka watu ndani zaidi ya muda uliwekwa kisheria.
Lakini watanzania wengi hawajua hili…hii inatokana na uelewa finyu wa
naswala ya kisheria,” alisema Mchemgerwa, wakati wa ufunguzi wa
kongamano hilo liloandaliwa na Shirika la Legal Services Facility (LSF).
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohamed Mchengerwa akifungua kongamano la siku mbili la kitaifa la msaada wa kisheria kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani linalofanyika mjini Dodoma.
Alisema wapo watu ambao wanakutana na matatizo mbalimbali pamoja na kuwekwa ndani bila ya makosa kutokana na kutokujua sheria.
Mchengerwa
alisema watu wengi hawajui kama kuna dhamana ya polisi ambapo mtuhumiwa
hatakiwi kukaa mahabusu zaidi ya saa 24 bila kupelekwa mahakamani au
kupewa dhamana.
Katika
kongamano hilo,Mchengerwa alisema watoa msaada wa kisheria wanatakiwa
kutoa msaada huo katika kila wilaya hususani maeneo ya mjini na
vijijini.
“Wapo watu ambao wako gerezani na hawana kosa lakini kutokana na tatizo la uelewa mdogo wa kisheria wamekuwa wakifungwa.
Abdullkarim Saidi, mmoja watoa msaada wa kisheria kutoka Zanzibar akizungumza kwa niaba ya wasaidizi wa kisheria wa visiwani Zanzibar.
“Jamii
bado haijui kama kuna dhamana ya polisi pia ni kosa la kisheria kumweka
mahabusu mtuhumiwa zaidi ya saa24 bila kumpeleka mahakamani au kumpatia
dhamana”alieleza.
Aliwataja
wasaidizi wa kisheria kama nguzo muhimu ya kuwasaidia kuelemisha
watanzania kuhusu maswala haya ya kisheria na jinsi ya kupata haki zao
pindi wanapopatwa na matatizo mbalimbali ya kisheria.
Kwa
upande wake mmoja wa watoa msaada wa kisheria kutoka Zanzibar,
Abdullkarim Saidi alisema licha ya kazi kubwa wanayofanya ya kutoa
msaada wa kisheria, wasaidizi wa kisheria nchini bado wanakabiliwa na
changamoto nyingi.
Washiriki wa Kongamano la Kitaifa la Wasaidizi wa Kisheria walioshiriki kongamano hilo linalomalizika mjini Dodoma leo.
Alisema
changamoto hizo ni pamoja na kukosekana kwa usafiri pamoja na fedha za
kuendesha shughuli zao kwa ufanisi, na kuongeza kuwa “tunafanya kazi
katika mazingira ambayo si rafiki kutokana na kutembea kwa umbali
mrefu.”
Kwa
upande wake, Mtendaji Mkuu wa LSF Bw. Kees Groenendijk amesema shirika
lake limeweka mikakati madhubuti ya kuwasaidiza wasaidizi wa kisheria
waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi, ikiwa ni pamoja na
kuwawezesha kifedha na kitaaluma ili waweze kuwasaidia na kuwafikia
watanzania wengi zaidi wenye matatizo mbalimbali ya kisheria.
Kwa
mujibu wa Kees, mpaka sasa shirika la LSF limeshatoa zaidi ya shilingi
billion 20 kwa mashirika mbalimbali yanajishughulisha na utoaji wa
huduma za kisheria—lengo kuu likiwa ni kuwasaidia watanzania kupata haki
zao.
Ramadhani Masele, Progamme Meneja wa LSF, akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Kongamano la wasaidizi wa kisheria Dodoma.
Wasaidizi wa kisheria wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa uzinduzi wa kongomano la wasaidizi wa kisheria Dodoma.
Scholastica Jullu, Programme Meneja wa LSF, akiongea wakati wa Kongamano la wasaidizi wa kisheria Dodoma.
Wasaidizi wa Kisheria wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa Kongamano la wasaidizi wa kisheria lililofanyika siku mbili mjini Dodoma 25-26, 2016 na kumalizika leo.


0 comments :
Post a Comment