Baada
ya mapumziko ya siku moja, kikosi cha Mbeya City Fc leo kimeanza rasmi
mazoezi kujiweka sawa tayari kwa mchezo mwingine wa ligi kuu ya soka
Tanzania bara dhidi ya Simba Sc uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa
Sokoine jumatano ijayo hii ikiwani siku tano tu baada ya suluhu ya
bila kufungana na Stand United.
Muda
mfupi uliopita Ofisa habari, Dismas Ten ameimbia mbeyacityfc.com
kuwa, nyota kadhaa waliokosa michezo miwili iliyopita kutokana na
majeraha wamekuwa sehemu ya kikosi kilichofanya mazoezi asubuhi ya leo
tayari kwa kuivaa Simba Sc siku ya jumatano.
“Haruna
Shamte na Sankhani Mkandawile wamekuwa sehemu ya kikosi kilichofanya
mazoezi leo asubuhi, hii ni tafsiri kuwa kikosi chetu kimetimia,Simba ni
timu ambayo tunaijua, hatuna shaka nao mara kadhaa wamekuja hapa
wakapata kipigo, tunafahamu wamekuwa na mwanzo mzuri wa msimu lakini
kucheza na City ni jambo tofauti inawalazimu kujipanga sana, waje
nasisi tupo tayari” alisema.
Akiendelea
zaidi Ten alisema kuwa, kikosi chake kilicheza vizuri mchezo uliopita
dhidi ya Stand United na kufanikiwa kutawala mchezo wa dakika zote
lakini safu ya ushambuliaji haikuwa na baati licha ya kujaribu mara
kadhaa kupiga mashuti yaligonga mwamba.
“Tulikuwa
na mchezo mzuri dhidi ya Stand, kwenye soka wakati mwingine bahati huwa
ina nafasi yake, Simba wajiandae vya kutoasha kwa sababu tumedhamiria
kufunga magoli mengi,tunajua tabia zao wanapofungwa lakini uwanja wa
Sokoine una sura nyingine, jambo muhimu kwa waamuzi tunaomba wachezeshe
mchezo kwa kufuata sheria 17, ili mashabiki wapate burudani na
kufurahia ushindi kwa timu yao”, alimaliza.


0 comments :
Post a Comment