Wanafunzi
wa upolisi na walinzi 58 wa Chuo cha Polisi Balochistan kilichopo
Quetta, Pakistan wanaripotiwa kupoteza maisha baada ya kutokea mlipuko
chuoni ambao unakisiwa kufanywa na wanamgambo.
Taarifa
zinaeleza kuwa walionekana wanamgambo watatu wakiingia eneo la chuo
wakiwa wamefunika sura zao huku wakiwa wamevaa mabomu ambayo waliyatumia
kufanya mlipuko.
Baada
ya shambulizi hilo, polisi wengine waliokuwa eneo hilo walifanikiwa
kuwashambulia watu hao na kuwaua na mpaka sasa hakuna kikundi chochote
ambacho kimejitangaza kuhusika na shambulizi hilo.
Mamia
ya wanafunzi wa chuo hicho wamehamishwa kutoka katika chuo hicho cha
upolisi cha Balochistan na polisi wameongezwa eneo la chuo ili
kuimarisha ulinzi.
Akizungumza
kuhusu tukio hilo, mmoja wa wanafunzi ambao walilishuhudia alisema,
“Niliwaona wanaume watatu wakiwa wamefunika sura zao na wakiwa wameficha
silaha aina ya kalashnikovs, walianza kupiga risasi katika mabweni na
mimi nilikimbia kwa kuruka ukuta”


0 comments :
Post a Comment