Watu
12 wanaripotiwa kupoteza maisha wakiwa katika nyumba ya kulala wageni
(Bishaaro Hotel lodge) katika mji wa Mandera, Kenya baada ya wapiganaji
wa kikundi cha Al Shabab kuvamia katika nyumba hiyo na kufanya
shambulizi usiku wa kuamkia leo.
Kamanda
wa Polisi wa Mandera Mashariki, Ezekiel Singoe amethibitisha kutokea
kwa vifo hivyo na kuwa watu 10 kati ya waliouliwa ni wanafunzi ambao
walikuwa wamefanya vizuri katika masomo yao ya sekondari na walikuwa
katika mji huo kwa ajili ya kukabidhiwa vyeti vyao.
Singoe amesema kwa sasa bado miili ya marejemu haijafahamika na ndugu zao na taratibu zinaendelea.
Amesema
watu hao walipofika katika nyumba hoteli hiyo walitumia mlipuko kuvunja
mlango kisha kuingia ndani ambao waliingia katika vyumba ambavyo
walikuta watu na kuwaua.


0 comments :
Post a Comment