November 10 2016 wabunge wa Bunge la
Afrika Kusini wamefuta kabisa pendekezo la kupiga kura ya kutokua na
imani dhidi ya Rais wa Afrika Kusini wa nchi hiyo Jacob Zuma pamoja na
kuwepo madai ya hivi karibuni kuhusu ufisadi na matumizi mabaya ya
madaraka kwa kiongozi huyo.
Kwa mujibu
wa Radio France International, Uchunguzi uliofanywa na tume ya
kukabiliana na ufisadi nchini Afrika Kusini umesema kuwa jopo la majaji
linatakiwa kuundwa ili kuchunguza madai ya uhalifu katika serikali za
Rais Zuma.
Uchunguzi
huo ulipata ushahidi kwamba familia tajiri ya mfanyabiashara Gupta yenye
uhusiano mkubwa na Zuma huenda ilikuwa na ushawishi mkubwa katika
uteuzi wa baraza la mawaziri wa Afrika Kusini.
Taarifa
iliyotolewa baada ya uchunguzi wa tume ya kukabiliana na ufisadi nchini
humo wiki iliopita ilizua madai ya kutokuwepo kwa nidhamu ya madaraka
dhidi ya Rais Jacob Zuma.
Baada ya
kupigwa kura za kutoa mapendekezo ya kutokua na imani na Rais, Chama cha
Rais Zuma ANC chenye wabunge wengi katika bunge na mswada huo wa
upinzani kilishinda kwa kura 214 dhidi ya 126 za upinzani.
Hii ni
imekua ni mara ya tatu kwa Rais Zuma kupigiwa kura na wabunge kutokuwa
na imani naye kulikofanywa bungeni katika kipindi kisichozidi mwaka
mmoja.


0 comments :
Post a Comment