Melanie Trump ambaye ni mke halali
Rais mteule wa Marekani Donald Trump, alizaliwa April 26,1970 mjini
Novo Mesto Yugoslavia. Alizaliwa na kupewa jina la Melanija Knavs baadae
akabadilisha kuwa Melania Knauss.
Melania Trump
Baba yake alikuwa anajishughulisha na
biashara ya magari huku mama yake akiwa mwanamitindo na mtengenezaji wa
nguo za watoto. Aliishi kwenye familia ya kawaida akiwa na mdogo wake wa
kike mpaka baadae alipogundua kuwa na kaka mkubwa ambaye baba yake
alimpata kwenye mahusiano kabla ya kuwa na mama yake.
Tasnia ya urembo & Elimu
Alipofikisha maika 16 akaanza
kujihusisha na mambo ya fashion na mitindo, baada ya miaka miwili
akasajiliwa kwenye moja ya mashirika yanayojihusisha na mitindo huko
Milan. Japokuwa alikuwa akiendelea na masomo katika chuo cha Ljubljana,
aliacha shule ili aweze kuendeleza kipaji chake, ingawa Tangu mwaka 2006
Melanie amekuwa akisema alishamaliza Degree yake ya masomo ya Uhandisi
chuoni hapo.
Mwanzoni alikuwa akifanya kazi mjini
Milan na Paris kabla ya kuhamia New York mwaka 1996 ambapo ndipo
alipopata makazi ya kudumu kikazi na aliweza kufanya kazi na wapiga
picha maarufu kama Patrick Demarchelier na Helmut Newton huku akitokea
kwenye kurasa za mbele za majarida makubwa ya fashion.
Melania na Donald Trump kwenye harusi yao 2005 -Palm Beach Florida
Kukutana na Donald Trump mpaka Ndoa
Mwaka 1998 Melania alikutana na Donald
Trump huko New York katika party ya fashion, japokuwa mwanzoni alimtolea
nje Trump, baadae wakaelewana na kuanza kuweka mahusiano yao hadharani
na mwaka 2004 Trump akamvisha pete ya uchumba. Mwaka uliofuata 2005
wakafunga ndoa huko Palm beach Florida, sherehe ambayo ilihudhuriwa na
mastaa wakubwa, pamoja na Rais Bill Clinton na mkewe Hillary Clinton
ambaye wakati huo alikuwa seneta kwenye jimbo la New York.
Melania, Donald Trump na mtoto wao Barron
Mwaka 2006 Melania alijifungua mtoto wa
kwanza, Barron William Trump ambaye kwa Trump yeye ni mtoto wa tano.
Mwaka huo huo Melania akawa raia rasmi wa Marekani.
Wakati wa Kampeni za Urais
Wakati Donald Trump alipotangaza nia ya
kugombea nafasi ya uraisi 2016, kama ilivyokuwa kwa Michelle Obama,
Melanie alianza kujihusisha na jamii huku akipokea maoni mabaya
yaliyokuwa yakihusisha picha za utupu alizowahi kupiga wakati akiwa
model mwaka 2000 huku raia wakilalamika kuwa sio mfano wa kuigwa kwa
jamii kutokana na picha zake nyingi za utupu zilizosambaa mitandaoni.
Maneno hayakuishia hapo, July 2016
Melania alitoa hotuba makao makuu ya chama cha Republican ambayo maelezo
mengi yalifanana na yale ya Michelle Obama wakati alipokuwa akitoa
hotuba yake 2008 makao makuu ya chama cha Democratic Marekani ambapo
iliibua mjadala mkubwa kwenye vyombo vya habari.
July 2016 Melania Trump alipokuwa akitoa hotuba yake iliyofananishwa na ile ya Michelle Obama
Baadae
mwandishi wa Trump Meredith McIver, akakiri kukosea na yeye ndiye
alichanganya kwa bahati mbaya ripoti ya Melanie na baadhi ya maneno
yaliyokuwepo kwenye hotuba ya Michelle. Mwezi huo huo july 30,2016
gazeti la Ney York Post likachapisha picha za utupu za Melania Trump
akiwa na miaka 25, ambapo alionekana akiwa na mwanamke mwenzake, picha
ambayo baadae ilifutwa.
Baada ya
sekeseke hilo Trump aliwajibu The New York Post kuwa Melania ni moja
kati ya models wenye mafanikio makubwa na amepiga picha nyingi kwenye
covers za majarida makubwa na picha hiyo ilichapishwa kwenye jarida la
Uingereza na ndilo lilimuwezesha kumfahamu Melania.
Cover la jarida la Vogue baada ya harusi ya Melanie na Donald Trump
November 2016, Melanie alitoa hotuba
fupi wakati wa kampeni na akieleza ni kitu gani atakachofanya ili kuzuia
matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii kama atakuwa first lady wa
Marekani na kusema kuwa ‘Tunapaswa tunapaswa tuwafundishe vijana
wetu maadili ya kimarekani, wema, uaminifu, heshim, huruma, upendo,
maelewano na ushirikiano’
Melania ana duka kubwa maarufu la vito vya thamani pamoja na bidhaa za ngozi.
Aidha ameshawahi kutangaza kipindi maarufu cha The View pamoja na kuonekana katika Reality Tv Show ya mumewe inayoitwa Celebrity Apprentice.
Kingine kutoka kwa Mke wa Rais Mteule
Melania Trump ni kwamba na uwezo wa kuongea vizuri lugha tano ikiwemo
Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, Kislovenia na Kiserbia.


0 comments :
Post a Comment