Prof. Mbarawa Kumuwakilisha Rais Magufuli Mkutano Wa Usafirishaji Duniani


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano wa kimataifa wa Usafirishaji Duniani utakaofanyika katika mji wa Ashgabat nchini Turkemistan kuanzia tarehe 26-27 Novemba, 2016.

Ajenda kuu ya mkutano huo ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambao utashirikisha viongozi mbalimbali utajadili kwa kina maeneo muhimu ya ushirikiano wa kimataifa kwenye Sekta ya Usafirishaji kwa maendeleo endelevu Duniani.

Aidha katika mkutano huo Waziri Prof. Mbarawa atapata fursa ya kukutana na wawekezaji mbalimbali Duniani waliobobea katika sekta ya usafirishaji na kuwashawishi kuwekeza hapa nchini.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment