Liverpool Imechezea Kichapo Cha Nne Mtungi Kutoka Kwa Bournemouth

licha

Wakicheza bila kiungo wao mshambuliji Philipe Countinho timu ya Liverpool imeangukia pua baada ya kukubali kichapo cha magoli 4-3 dhidi ya Bournemouth mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza kwenye uwanja wa Vitality .

Licha ya kuongoza magoli mawili kipindi cha kwanza ambayo Liverpool waliyapata kupitia kwa Saido Mane dakika ya 20 na dakika ya 22 Divock Origi alifunga la pili hadi mapumziko wageni walikuwa mbele kwa mawili.

Kipindi cha pili kilikuwa kibaya kwa Jurgen Klopp kocha wa Liverpool kwani timu ya Bournemouth waliingia uwanjani kama nyuki aliyejeruhiwa huku katikati ya dimba kiungo toka Arsenal kwa mkopo Jack Wilshere akilitawala na dakika ya 56 Wison alifunga goli la kwanza kwa wenyeji.

Liverpool walifunga goli la tatu lililofungwa na Emer Can baada ya kuongoza magoli matatu kwa moja Bournemouth walijipanga kikamilifu na waliweza kupata magoli ya haraka haraka kupitia kwa Fraser dakika ya 76,mshambuliaji Cook alisawazisha la tatu na ubao kusomeka 3-3 zikiwa zimesalia dakika za majeruhi Ake alipingilia msumari wa nne na kuwanyamazisha mashabiki wa Liverpool.

Hadi mwamuzi anamaliza mpira Liverpool wametandikwa kwa aibu jumla ya magoli 4-3 na kwa Matokeo hayo Liverpool wanabaki nafasi ya tatu wakiwa na pointi 30 wakati Bournemouth wamepanda hadi nafasi ya 10 wakiwa na pointi 18 ya msimamo na kinara wa Ligi ni Chelsea wenye pointi 34.

VIKOSI:Bournemouth (4-3-3): Boruc; Smith, Francis, Cook, Ake, Artur, Gosling (Afobe 75), Wilshere, Stanislas (Fraser 53), King (Ibe 46), Wilson

Subs not used: Federici, Mings, Smith, Pugh

Goals: Wilson (56), Fraser (76), Cook (79), Ake (90+1)

Bookings: Wilshere (48), Francis (50)

Liverpool (4-3-3): Karius; Clyne, Lucas, Lovren, Milner, Can, Henderson, Wijnaldum, Origi, Mane (Lallana 79), Firmino

Subs not used: Mignolet, Alexander, Ejaria, Woodburn, Moreno, Klavan

Goals: Mane (20), Origi (22), Can (63)

Bookings: Henderson (53)

Referee: Bobby Madley

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment