Shirikisho la soka Tanzania TFF leo December 7 2016 limetoa taarifa kuhusu wale marefa Martin Saanya na Samwel Mpenzu waliochezesha mchezo wa 49 wa Ligi Kuu soka Tanzania bara kati ya Yanga na Simba uwanja wa Taifa Dar es Salaam na mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
Maamuzi yaliofanywa katika kikao cha uendeshaji wa bodi ya Ligi imeamua kuwaondoa marefa Martin Saanya na Samwel Mpenzu katika ratiba ya uchezeshaji wa mechi za Ligi Kuu msimu wa 2016/2017 na kupelekwa katika kamati ya waamuzi ili suala lao lishughulikiwe kitaalam.
Hata hivyo kikao hicho pia kimemuondoa refa aliyechezesha mechi namba 108 kati ya Mbeya City na Yanga Rajab Mrope na kumrudisha kwenye kamati ya waamuzi ili wampangie daraja lingine, Mrope amekutwa na hatia ya kosa la kutojihamini mchezoni.
0 comments :
Post a Comment