Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha Profesa Ibrahim
Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
aliyefika Chato mkoani Geita kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Profesa Ibrahim
Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais wa Nigeria Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akipokea barua yenye ujumbe maalum kutoka kwa
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari uliowasilishwa na Profesa Ibrahim
Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais huyo wa Nigeria, Chato mkoani
Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Profesa Ibrahim
Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari mara
baada ya kumaliza mazungumzo yao Chato mkoani Geita.
Profesa Ibrahim Gambari ambaye ni Mjumbe
maalum wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari akimshukuru Rais Dkt. John
Magufuli mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mgeni wake Profesa Ibrahim Gambari
ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari mara baada
ya kumaliza mazungumzo yao Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Profesa Ibrahim Gambari
ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari mara baada
ya kumaliza mazungumzo yao Chato mkoani Geita. PICHA NA IKULU.
………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 10 Januari, 2017 amekutana
na kufanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Rais wa Nigeria Profesa
Ibrahim Gambari nyumbani kwake Chato Mkoani Geita. Mazungumzo yao
yalilenga masuala mbalimbali ya uhusiano kati ya Tanzania na Nigeria.
Rais Magufuli amempongeza Rais Muhammadu Buhari kwa jitihada kubwa anazochukua kwa ajili ya kuleta maendeleo nchini mwaka.
Pia, Rais Magufuli amempongeza
Rais Buhari kwa jitihada anazozifanya za kukabiliana na kundi la Boko
haramu ili kuhakikisha amani inaendelea kudumu nchini mwake.
Kwa upande wake Mjumbe Maalum wa
Rais wa Nigeria, Profesa Ibrahim Gambari amempongeza Rais Magufuli kwa
ushindi alioupata na jitihada anazochukua katika kupambana na rushwa na
kubana matumizi jambo ambalo linaungwa mkono na wananchi wengi wa
Nigeria.
Profesa Gambari alimkabidhi Rais Magufuli barua yenye ujumbe maalum kutoka kwa Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato, Geita
10 Januari, 2017
0 comments :
Post a Comment