WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imelipa jumla ya sh. bilioni 29
kwa watumishi mbalimbali wa umma wakiwemo walimu ikiwa ni sehemu ya
madeni yao.
Alitoa
kauli hiyo jana (Jumamosi, Januari 21, 2017) wakati akizindua vyumba
vitatu vya kisasa vya madarasa katika shule ya sekondari Iwawa iliyoko
wilayani Makete.
Waziri
Mkuu alisema Serikali imedhamiria kumaliza madeni ya watumishi hao,
ambapo hadi kufikia Novemba mwaka jana jumla sh. bilioni 29 zililipwa
kwa watumishi 31,000.Alisema kwa sasa Serikali imejipanga kuhakikisha
hakuna madeni mapya yanayozalishwa hivyo amewataka watumishi wa umma na
wananchi kuendelea kuiunga mkono Serikali.
Hata
hivyo alisema Serikali inaendelea na mikakati ya kuboresha sekta ya
elimu kwa kujenga mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia.“Tumeanza
mradi wa ujenzi wa nyumba za walimu katika halmashauri nchini. Hapa
Makete tumeleta sh. milioni 557 kwa ajili ya ujenzi huo,” alisema.
Alisema
nyumba hizo za walimu zinazojengwa katika maeneo mbalimbali hususan ya
vijijini ni za kisasa ambazo zinalenga kuwaondolea changamoto ya
makazi.Waziri Mkuu alisema Serikali inafanya jitihada za dhati za
kuhakikisha kila Mtanzania anapata elimu kwa kuwa elimu ni kichocheo cha
maendeleo ya jamii.
“Tumedhamiria
kumpatia elimu kila Mtanzania, hivyo halmashauri zihakikishe kila
kijiji kinakuwa na shule ya msingi na lazima ziwe na darasa la awali,”
alisema.Naye Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Novatus Msivala aliishukuru
Serikali kwa kugharamia ujenzi wa vyumba hivyo vitatu vya madarasa na
matundu 10 ya vyoo pamoja na uingizaji wa maji kwenye vyoo na
utengenezaji wa madawati 46.
Alisema
ujenzi huo umegharimu sh. milioni 95 ambao utasaidia kupunguza
msongamano kwa wanafunzi. Kwa sasa Serikali na wananchi wanaendelea
kukamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi ya walimu.
Katika
hatua nyingine jana Waziri Mkuu alitimiza ahadi yake ya kumpatia laptop
mwanafunzi Ally Alijai wa Chuo kikuu cha SAUT tawi la Songea mkoani
Ruvuma.Ahadi hiyo aliitoa mwanzoni mwa mwezi huu alipokuwa katika ziara
yake kikazi mkoani Ruvuma, lengo likiwa ni kuendeleza kipaji cha utunzi
wa vitabu kwa mwanafunzi huyo.
Alisema
mwanafunzi huyo alionyesha umahiri mkubwa katika utungaji wa kitabu
ambacho kinaweza kutumika kufundishia katika shule za sekondari.
Hata
hivyo Waziri Mkuu alisema tayari kitabu hicho kimeshawasilishwa Taasisi
ya Elimu Tanzania (TEA) kuona kama kinaweza kuanza kutumika kwa
kufundishia. Mwanafunzi huyo alishukuru kwa zawadi hiyo na kuahidi
kutunga vitabu vizuri zaidi.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JANUARI 22, 2017.
0 comments :
Post a Comment