Baada ya kukosekana kutokana na majeruhi, Samatta karudi uwanjani na kuifungia KRC Genk


Mtanzania Mbwana Samatta ambaye anaichezea KRC Genk ya Ubelgiji, usiku wa February 10 2017 aliingia uwanjani kuichezea timu yake dhidi ya Santi Truiden.
Samatta ambaye alikuwa majeruhi toka January 31 2017 katika mchezo wa nusu fainali ya Crocky Cup dhidi ya KV Oostende uliyomalizika kwa KRC Genk kuondolewa katika michuano hiyo kwa goli 1-0, amerudi uwanji kuendelea kutumikia timu yake.

Nahodha huyo wa Taifa Stars amerudi katika timu baada ya kukosa mechi mbili ukiwemo mchezo aliyoumia ambao alicheza kwa dakika 24 pekee, leo ameisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa goli 3-0, Samatta akifunga goli la pili dakika ya 40 baada ya Alejandro Pozuelo kufunga goli la kwanza dakika ya 37 na Ruslan Malinovskiy kuhitimisha kwa kufunga goli la tatu dakika ya 45.

Ushindi huo unaifanya KRC Genk kutimiza jumla ya point 41 katika msimamo wa Ligi Kuu Ubelgiji wakiwa wamecheza jumla ya michezo 26, kwa sasa wapo nafasi ya tano katika msimao wa Ligi hiyo inayoshirikisha timu 16 lakini matumaini ya kupata nafasi za kucheza play off za UEFA yapo kutokana na ushindi huo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment