HOMA
ya pambano la watani wa jadi Simba na Yanga limeanza kupanda ambapo
baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wameanza kutambiana huku kila mmoja
akimtahadharisha mwenzake kuelekea kwenye mchezo huo.
Pambano hilo linalosubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki limepangwa kuchezwa Februari 25 kwenye Uwanja wa taifa.
Kikosi cha Yanga kiliwasili jana mchana kikitokea Comoro walipokwenda kucheza mchezo wao wa kwanza wa hatua ya awali ya klabu bingwa Afrika.
Nyota wa timu hiyo, Haruna Niyonzima, aliiambia Nipashe kuwa ushindi walioupata Comoro dhidi ya Ngaya de Mde, umewaongezea molali kuelekea kwenye mchezo wao dhidi ya Simba.
"Hatuna hofu na mchezo wowote, mchezo na Simba tunauchukulia uzito sawa na michezo mingine tu.., naamini kikosi chetu kipo vizuri zaidi," alisema Niyonzima.
Kwa upande wake, nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub 'Cannavaro' alisema mashabiki wa timu hiyo wasiwe na hofu na kwa kuwa wanajipanga kwa ajili ya ushindi.
"Tumerejea kujiandaa na michezo yetu ya mbele ukiwemo huo dhidi ya Simba.., tutarejea kileleni na hatuihofii Simba," alisema Cannavaro.
Wakati Yanga wakitamba kuelekea kwenye mchezo huo, nahodha wa Simba, Jonas Mkude, alisema hawatarajii kushuka kileleni mwa msimamo wa ligi.
"Tunafahamu umuhimu wa mchezo wetu na Yanga.., makocha wetu wanajua nini cha kufanya kuhakikisha tunapata pointi tatu, hatuna sababu ya kuhofia Yanga," alisema Mkude.
Ugumu wa mchezo huo unatokana na upinzani uliopo kwenye msimamo wa ligi kuu ambapo Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 51 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 49 lakini ikiwa na akiba ya mchezo mmoja ukilinganisha na Simba iliyocheza michezo 22.
Kwa kiasi kikubwa hatma ya ubingwa msimu inategema zaidi matokeo ya mchezo huo wa watani wa jadi.

About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments :
Post a Comment