KAULI YA KWANZA YA SERIKALIKUHUSU WATANZANIA WALIOTIMULIWA MSUMBIJI


Kumekuwepo na taarifa mpaka za video Watanzania mbalimbali wakiongea baada ya kuondolewa kwa lazima nchini Msumbiji na kurudishwa Tanzania kwa Malori huku wengine wakisema Polisi wa Msumbiji wamewanyang’anya simu na pesa walizokua nazo.

Leo Wizara ya mambo ya nje ya Tanzania kupitia Naibu waziri wake imetoa ufafanuzi kuhusu ishu hii kwa kusema “Mnajua kabisa uhusiano wa Tanzania na Msumbiji sio mbaya na hata December 2016 tulifanya mkutano na kutazamia maswala ya uhusiano na biashara
Baada ya kusikia taarifa za kukamatwa na kuondolewa kwa Watanzania, tulituma ubalozi wetu kujua ni kitu gani kinaendelea na wameambiwa Serikali ya nchi hiyo inawaondoa walioingia kwenye taifa hilo isivyo halali

Ubalozi wetu kwa Msumbiji wako pale wanashirikiana na serikali ya Msumbiji, uongozi wa Mtwara na UHAMIAJI Mtwara pia wako pale wanashughulikia… tunachokifanya sasa hivi ni kuhakikisha kama ni kweli yale yaliyosemwa na Watanzania ikiwemo kunyang’anywa hati za kusafiria

“Tumeambiwa zoezi hilo la Msumbiji sio tu kwa raia wa Tanzania bali raia wa nchi mbalimbali walioingia nchini humo bila vibali au kufata taratibu za kuishi na kufanya kazi nchini humo“
Naibu Waziri ameahidi kutoa taarifa kamili baadae lakini ya kufahamu kwa sasa ndio hayo
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment