CHANZO BBC
Misri
imeweka rekodi kwa kufanikiwa kufuzu kwa mara ya tisa katika fainali za
kombe la Afrika baada ya kuishinda Burkina Faso 4-3 katika mikwaju ya
penalti baada ya sare ya 1-1.
Mlinda lango wa miaka mingi Essam
El Hadary alithibitisha ushujaa wake kwa kuokoa penalti iliopigwa na
Betrand Traore ili kupata ushindi huo.
Wakati wa muda wa kawaida Mohamed Salah aliiweka kifua mbele Misri baada ya kufunga bao zuri.
Hatahivyo Burkina Faso walisawazisha wakati Aristide Bance alipofunga krosi iliopigwa na Charles Kabore.
Kupitia bao hilo Burkina Fasso imekuwa timu ya kwanza kuifunga Misri katika mchuano huo.
Wachezaji wa Burkinabe ambao ndio
walioonyesha mchezo mzuri wakati wa muda wa kawaida walianza penalti
hizo kwa kufunga, lakini Misri ikaibuka mshindi baada ya Traore
kushindwa kucheka na wavu.
0 comments :
Post a Comment