Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye ameingilia
kati na kutaka busara itumike katika zoezi la kutaja wasanii wanaohusika
na dawa za kulevya linalofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda
Nape ametoa ushauri huo leo Mjini Dodoma wakati akizungumza na
wanahabari kuhusu sheria mpya wa huduma za habari, ikiwa ni siku nne
tangu mkuu huyo wa mkoa aanze kutaja wahusika wa dawa za kulevya
wakiwemo wasanii wa bongo fleva na filamu.
Baadhi ya waliotajwa na kutakiwa kuripoti polisi kwa mahojiano ni pamoja
na Vanessa Mdee, Wema Sepetu, Nyandu Toz, Chidi Benz, TID, Tunda, Babuu
wa Kitaa n.k
Nape baada ya kuulizwa swali na wanahabari kuhusu suala hilo amesema
kuwa wizara yake inakiri kuwa tatizo hilo ni kubwa, na ilifikia hatua ya
kuwasaidia baadhi ya wasanii kwenda kupata matibabu akiwemo msanii Ray C
na kwamba wanaunga mkono jitihada zozote za kupambana na tatizo hilo.
Amesema tatizo lipo kwenye namna ya kuwaadhibu wanaogundulika kutumia
dawa za kulevya, kwa maana ya sheria ipi itumike kuwashitaki, lakini pia
tatizo lingine ni busara inayotumika kuwataja na kuwakamata watu ambao
tayari wamekwisha athirika na dawa kulevya badala ya kuwasaidia.
Kwa mtazamo wake nape amesema hilo ni tatizo la jamii nzima, na kushauri
jamii yote ya watanzania kushiriki katika kujenga maadili ya watoto.
0 comments :
Post a Comment