SIMBA YAKOLEZA KASI YA UBINGWA VPL,YAITANDIKA MAJIMAJI KAPU LA MAGOLI


MAVUGO NA KICHUYA
Timu ya Simba imekoleza mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania baada ya kuifanyia mauaji Majimaji kwa kuifunga goli 3-0 Mchezo uliochezwa uwanja wa Majimaji Mjini Songea mkoani Ruvuma.
Alikuwa Ibrahim Ajibu Migomba aliwanyanyua mashabiki wa Simba dakika ya 19 akifunga bao kwa kichwa akimalizia pasi ya Shiza Kichuya hadi Mapumziko Simba walikuwa mbele.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko hata hivyo Simba waliweza kunufaika na mabadiliko hayo Said Ndemla alifunga bao la pili kwa Mkwaju Mkali dakika ya 64 na kumuacha mlinda mlango wa Majimaji hana la kufanya.
Dakika ya 88 Laudit Mavugo aliandika kalamu ya magoli kwa kufunga bao safi hadi mwamuzi anamaliza Mpira Simba wameibuka na pointi tatu na kuendelea kushika nafasi ya pili.
Kwa Matokeo hayo Simba wamefikisha Pointi 48 nyumba ya Yanga wenye pointi 49 Ligi hiyo inatarajia kuendelea kesho kwa Timu ya Azam Fc kucheza na Ndanda kwenye dimba la Azam Complex Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment