Wachimbaji 13 waliokolewa tarehe
hiyo hiyo 13 Februari, 2017 wakiwa hai na kupelekwa katika Hospitali ya
Wilaya ya Butiama kwa matibabu. Zoezi la kutafuta wachimbaji wengine
liliendelea ambapo tarehe 14 Februari, 2017 maiti mbili zilipatikana
katika shimo hilo. Juhudi zaidi zinaendelea kutafuta wachimbaji wengine
waliobaki ambapo Uongozi wa Wilaya ya Musoma kupitia Kamati ya Ulinzi na
Usalama pamoja na Wizara ya Nishati na Madini kupitia Ofisi ya Madini
Musoma kwa kushirikiana na Mgodi wa North Mara na Wachimbaji wadogo
wanaendelea na zoezi la uokoaji. Juhudi za kufukua shimo lililoporomoka
pia zinaendelea ili kuona kama kuna watu zaidi katika shimo hilo. Mgodi
wa North Mara umetoa msaada wa mashine ya kuvuta maji na tope ili
kuwezesha zoezi la ufukuaji kuendelea.
Wizara ya Nishati na Madini
inachukua fursa hii kuwatangazia Wananchi wote kuwa shughuli za
Utafutaji, Uchimbaji na biashara au shughuli yoyote ya madini
zinatakiwa zifanyike kwa kuzingatia Sheria ya Madini ya Mwaka 2010. Kwa
maana hiyo, lazima shughuli hizo zifanywe na wamiliki wa leseni na
vibali halali vinavyotolewa kwa mujibu wa sheria hiyo. Kwa kufanya
hivyo, itawezesha wataalam wa Wizara ya Nishati na madini kufanya
ukaguzi ili kuhakikisha kuwa shughuli hizo zinafanyika inavyotakiwa
ikiwa ni pamoja na usalama katika shughuli za uchimbaji.
Tunatoa wito kwa Wananchi wote
ikiwa ni pamoja na wachimbaji wadogo kuacha tabia ya kuvamia maeneo na
kuendesha uchimbaji katika eneo lolote bila kumiliki leseni kwa mujibu
wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010.
Imetolewa na;
KATIBU MKUU
WIZARA YA NISHATI NA MADINI


0 comments :
Post a Comment