Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limesikitishwa na taarifa iliyotolewa
na gazeti la Tanzania Daima toleo Nambari 4438 la tarehe 28 Januari
2017, Habari leo la tarehe 29 Januari 2017 na baadhi ya vyombo vya
habari vikihusisha mauaji ya kondakta wa daladala na Wanajeshi Mkoani
Tanga.
Tunapenda kuwataarifu wananchi
kwamba kwa mujibu wa jeshi la polisi watuhumiwa wanaoshikiliwa na Jeshi
hilo ni wanne (4),mmoja kati yao ni Mwanajeshi ambaye ni mzazi wa
msichana anayetuhumiwa kusababisha tukio hilo. Hivyo Mwanajeshi huyo
anashikiliwa kwa ajili ya kulisaidia Jeshi la Polisi katika uchunguzi
kwa kuwa tukio hilo lilifanyika nyumbani kwake. Hakuna Wanajeshi
waliohusika katika tukio hilo kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo
vya habari, kambi za Jeshi wanaishi Wanajeshi pamoja na familia zao
hivyo kuhusisha moja kwa moja mauaji hayo na Wanajeshi mkoani Tanga ni
kuupotosha umma.Wito unatolewa kwa vyombo vya habari kuripoti habari
zenye ukweli.Habari zisizo za kweli zinapotosha umma na kujenga taswira
potofu kwa wananchi dhidi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085
0 comments :
Post a Comment