Manji alifikishwa mahakamani hapo akitokea hospitali ya taifa ya Muhimbili alipokuwa kalazwa katika taasisi ya Jakaya Kikwete inayohusika na tiba za moyo, Manji amesomewa shitaka hilo na kukana na kesi yake imeahirishwa hadi March 16 2017.
Hata hivyo Manji kwa sasa ameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana, ambapo hakimu alimtaka ajidhamini mwenyewe kwa Tsh milioni 10 na mdhamini mmoja ambaye ataweka dhamana ya Tsh milioni 10 ambapo katibu mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa alijitokeza na kumdhamini.


0 comments :
Post a Comment