KIKOSI cha Mbeya City Fc
kimefanya mazoezi ya mwisho asubuhi ya leo kwenye uwanja wa shule ya
sekondari ya Kom mjini Shinyanga tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya
vodacom Tanzania bara dhidi ya Mwadui Fc uliopangwa kuchezwa kesho
Mwadui Complex.
Akizungumza na mbeyacityfc.com mapema leo, Ofisa habari wa kikosi hiki, Dismas Ten
amesema maandalizi yote kwa ajili ya mchezo huo yamekamilika asilimia
mia moja,hasa baada ya program za mazoezi kufanyika kwa siku mbili
kama ilivyokuwa imeelekezwa na kocha Kinnah Phiri na kinachosubiriwa
sasa ni dakika 90 za mchezo wa kesho.
Tumekuwa na siku mbili nzuri za mazoezi tangu tulipofika hapa Shinyanga siku ya juzi, tumekamilisha maandalizi yote tunasubiri dakika 90 za kesho, tunafahamu Mwadui ni timu nzuri lakini matokeo huja kulingana na vile ambavyo umejiandaa, sisi tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunashinda mchezo ili kupata pointi tatu, lengo letu ni kuona tunakuwa sehemu ya timu nne za juu mwisho wa msimu.
Akiendelea zaidi Ten alisema
nyota wote 20 walisafiri kwaa ajili ya michezo miwili ya kanda ya ziwa
wako kwenye hali nzuri pasipo majeraha yoyote kwa mujibu wa taarifa ya
daktari, na hakuna shaka kuwa wako tayari kuitetea timu yao kwa uhakika
na nguvu zote.
Tumesafiri na kikosi cha nyota
20, hii ni kwa sababu tuna mchezo mwingine dhidi ya Stand United wiki
ijao, asubuhi hii daktari wetu Guydon Makulila amesema wote wako
kwenye hali nzuri pasipo majeraha yoyote hivyo basi ni jukumu la benchi
la ufundi kuona nani na nani watakuwa sehemu ya kikosi cha kwanza
kwenye mchezo wa kesho na ulewa tutakaocheza Kambarage.
0 comments :
Post a Comment