Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) linachukua nafasi hii kuitakia kila la kheri timu ya
Young Africans katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo hatua
ya awali imeanza wikiendi hii.
Wakati Young Africans inacheza,
kesho Februari 12, mwaka huu huku Azam itasubiri mshindi kati ya Mbabane
Swallons ya Swaziland na Opara United ya Botswana katika michuano ya
Kombe la Shirikisho (CAF).
Timu ya Young Africans ambayo ni
mabingwa wa Tanzania inayoiwakilisha nchi katika michuano ya Ligi ya
Mabingwa Afrika, kesho Jumapili Februari 12, 2017 inacheza naNgaye De
Mbe ya nchini Comoro.
“Tunaitakia Wawakilishi wa nchi
Young Africans ya Tanzania kila la kheri,” amesema Rais wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi.
0 comments :
Post a Comment