MSIMAMIZI na Mwanasheria wa Mgodi wa RZ uliokuwa umewafukia watu 15
katika kijiji cha Mawe Meru kata ya Nyarugusu Wilaya na Mkoa wa Geita
Fransis Kiganga amesema watu hao walifukiwa na kifusi cha udongo kwenye
Mgodi huo watapata ajira na kufunga mkataba wa miaka miwili kila mmoja
wao.
Akizungumza na waandishi wa Habari juu ya watu hao 15 waliokuwa
wamefukiwa na kifusi kama wataendelaea na kazi ndani ya Mgodi huo au la,
Kiganga amesema kuwa wafanyakazi hao 15 baada ya kuokolewa na kupata
nafuu na Afya zao kuwa nzuri , watapatiwa mkataba wa miaka 2 kila mmoja.
Kiganga ameongeza kuwa Ofisi ya Madini Mkoa wa Geita imekuwa ikifanya ukaguzi wa kina na hicho kilichotokea ni ajali kazini.
Hivi karibuni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye ni
Mkuu wa Wilaya ya Geita Herman Kapufi aliitaka Kampuni hiyo kutoa
Mikataba kwa wafanyakazi wake huku waliookolewa wakiomba kuboreshewa
mazingira ya kazi.
0 comments :
Post a Comment