Aliembaka Mwenzie Nakumpa Ujauzito Ahukumiwa Kuchapwa Kiboko Kimoja



Mahakama ya Wilaya ya Hai  Mkoani Kilimanjaro  imetoa hukumu ya kuchwapwa kiboko kimoja mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Longoi wilaya hapo baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake wa shule hiyo.

Akisoma hukumu hiyo  Hakimu  mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Agnes Muhina  mbele ya mwendesha mashtaka wa polisi , Valeria Banda, alisema kuwa anatoa hukumu hiyo baada ya kuridhishwa na ushaidi uliotolewa mahakamani  hapo usioacha shaka yoyote.

Kesi hiyo pia ilikuwa na mashahidi sita wa upande wa mashtaka akiwemo daktari wa hospitali ya Hai,dawati la jinsia na watoto na mama mzazi wa binti huyo, mwalimu na binti mwenyewe.

Ilidaiwa na mwendesha mashtaka wa polisi  kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo   Oktoba 10, 2015 saa 8.00  mchana katika kijiji cha Mkalama Wilayani humo ambapo alimbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake wa kidato cha tatu mwenye umri (16).
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment