Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema taratibu zitafuatwa kuwawajibisha viongozi wake na wa serikali wanaokabiliwa na tuhuma na madai mbalimbali.
Polepole amesema hayo jana katika Makala ya Kinagaubaga, kipindi kinachorushwa na Idhaa ya Kiswahili ya Deutschen Welle(DW) baada ya kuulizwa swali kuhusu chama hicho kulea utovu wa nidhamu wa makada wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti wanaotuhumiwa kulidhalilisha Bunge na chombo hicho kwa kauli moja kutaka wajieleze.
Akijibu swali hilo Polepole alisema, "Ninyi hamkujua kama tutawachukulia watu juzi, Serikali ina utaratibu wake bunge lina utaratibu wake na chama kina utaratibu wake. Tunao utaratibu tunafuata, wananchi wawe na subira"
"Wananchi wawe na subira, ninafahamu wananchi wana subira sana, wasubiri mamlaka za viongozi, hawa wote waliokosea, mchakato wa haki ufanyike na hatimaye tutaona matunda yake."
0 comments :
Post a Comment