Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Magufuli, amepiga simu kwenye kituo cha runinga cha Clouds TV, wakati kipindi cha 360 kikiendelea na kueleza kuwa anampenda msanii Diamond Platnumz, anampongeza kwa kupata watoto na kuwa mwanachama wa CCM na kuahidi kushughulikia matatizo yanayowasumbua wasanii wa filamu na muziki Bongo.
Mheshimiwa Rais JPM alipiga simu moja kwa moja wakati kipindi kikiendelea, baada ya kumsikia Diamond aliyekuwa akihojiwa kwenye kipindi hiocho, akilalamika kwamba serikali imewatupa na haijali matatizo yao.
Mheshimiwa Rais akamhakikishia Diamond na wasanii wengine kwamba atashugulikia matatizo yao.
0 comments :
Post a Comment