Serikali Yapiga Marufuku Kufunga Ndoa Bila Kuwa Na vyeti Cha Kuzaliwa



Serikali imepiga marufuku watu kufunga ndoa bila kuwa na cheti cha kuzaliwa kuanzia Mei Mosi, mwaka huu.


Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe ametangaza utaratibu huo mpya hii leo, akiwa ziarani Mkoani Morogoro na kuongeza kwamba, serikali imeamua kufanya hivyo ili kupata takwimu sahihi za wananchi wake zitakazosaidia kupanga mipango ya kimaendeleo sawia na kuzuia wageni kuingia kinyemela nchini.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Mwakyembe ameitaka Wakala wa Usajili wa Vizazi na Vifo, (RITA), kuhakikisha inasimamia Sheria ya Usajili ambapo amesema, bila kuwa na takwimu sahihi za vizazi na vifo ama ndoa inasababisha nchi kushindwa kusonga mbele kimaendeleo.

Amesema, kwa mfano Mkoa wa Morogoro kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, inaonesha kuna jumla ya wakazi milioni 2.2, lakini waliosajiliwa na kuwa na vyeti vya kuzaliwa ni asilimia 11 pekee huku wengine wakiwa bado hawasajiliwa,
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment