Aliekuwa M/kiti Wa Ccm Mkoa Wa Iringa Ashikiliwa Na Jeshi La Polisi Iringa



Iringa. Jeshi la Polisi mkoani hapa linamshikilia mwenyekiti wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, kwa tuhuma za kumshambulia mwanamke mmoja na kumsababishia maumivu makali mwilini.

Msambatavangu, ambaye alikuwa miongoni mwa wanaCCM waliofukuzwa uanachama katika Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho uliofanyika mwezi Machi, amekamatwa mchana wa leo Alhamisi.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Julius Mjengi, amesema kuwa kiongozi mstaafu anatuhumiwa kutenda kosa hilo wiki iliyopita.

Akifafanua, Kamanda Mjengi alibainisha kuwa kiongozi huyo alitenda kosa hilo akiwa na wenzake ambao asingeweza kuweka majina yao hadharani kwani wanaendelea kuwatafuta.

"Ni kweli tunamshikilia Jesca Msambatavangu, tumemkamata leo saa nane mchana na tunaendelea na uchunguzi dhidi yake," alisema Mjengi na kuongeza:

"Jesca pamoja na wenzake wanatuhumiwa kumshambulia mwanamke mmoja mkazi wa Kibwabwa, walimshambulia na kisha kumchoma sindano ambayo mwanamke huyo hajui ni ya kitu gani," alisema Mjengi.

Alipohojiwa zaidi, Mjengi alikataa kuweka wazi jina la mwanamke na idadi ya watuhumiwa wengine kwa maelezo kuwa kufanya hivyo kunaweza kuharibu upelelezi unaoendelea.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment