JB Afunguka Kukosa Mtoto

Muigizaji maarufu wa filamu Bongo, Jacob Stephen  Bonge la bwana maarufu kama  JB amefunguka na kuweka wazi kwamba maisha yake ya kutopata mtoto mpaka sasa kwenye ndoa yake hayajawahi kumkosesha furaha wala kuacha kumpenda mke wake.
Kwenye kipindi cha Kikaangoni kupitia Facebook ya EATV wakati akijibu maswali ya mashabiki wake JB amesema kuwa hajabahatika kupata mtoto kwenye ndoa yake lakini bado hajakata tamaa na anaamini ipo siku Mungu atajibu maombi yake.

“Sina mtoto, sijabahatika kupata mtoto kwenye ndoa yangu, lakini kutokuwa na watoto kwenye maisha yangu haijawahi kunifanya nikose amani au nimchukie mke wangu. Nampenda sana lakini ipo siku naamini Mungu atatupatia au tusipopata kabisa sitaweza kukufuru kabisa” – JB.

Aidha JB ambaye amekiri kukaribia kufikisha umri wa miaka 50 amewataka watu wote ambao hawajajaliwa kupata watoto wasiache kumshukuru Mungu na siku zote waishi maisha ya furaha.

“Wakati mwingine nawaza kuna watu wamejaaliwa watoto lakini hawana furaha sisi tuliyonayo, niwaombe hata wale ambao bado hawajabahatika kupata watoto wasiishi kwa kukosa amani wafurahie maisha Mungu aliyowapatia watoto ni baraka itokayo kwa Mungu” – JB 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment