Yanga Yarejea Kileleni



Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
YANGA SC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Sifa nyingi kwa mfungaji wa bao hilo, Mzambia Obrey Chirwa dakika ya 70 baada ya kumtoka beki wa Azam FC, Mghana Yakubu Mohamed kufuatia pasi ndefu ya kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa wa kike mwenye beji ya FIFA, Deonesya Rukyaa wa Kagera, Yanga ilipata pigo dakika ya 30 baada ya kiungo wake Mzambia, Justin Zulu kuumia mguu wa kushoto na kushindwa kuendelea na mchezo nafasi yake kuchukuliwa na winga, Emmanuel Martin.
Mfungaji wa bao pekee la Yanga, Obrey Chirwa akimtoka beki wa Azam FC, Daniel Amoah leo Uwanja wa Taifa


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment