Wachezaji wasiopimwa afya kutoshiriki ligi msimu ujao

Wachezaji ambao hawatathibitishwa afya zao hawataruhusiwa kucheza katika ligi kuu Tanzania Bara, ligi daraja la kwanza pamoja na ligi daraja la kwanza msimu ujao wa 2017/18
Katazo hilo ni kwa mujibu wa mabadiliko ya kanuni za ligi hiyo yaliyofanywa na kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika kikao chake cha Julai 30 mwaka huu, ambacho pia kilipitisha mambo mbalimbali.
Katika mabadiliko hayo, mchezaji atakayesajiliwa hatapewa leseni ya kumruhusu kucheza mashindano husika kama hatakamilisha masharti makuu matatu.
Masharti hayo ni kukatiwa bima ya matibabu, kuidhinishwa afya yake ambapo fomu yake itapaswa kupitishwa na kamati ya tiba ya TFF na sharti la tatu ni kuwasilisha TFF mkataba wake wa maandishi ‘hardcopy’.
Kuhusu suala la mikataba, kanuni ya 69 (8), imeendelea kusisitiza kwamba: “Mikataba yote ya wachezaji ambayo haijasajiliwa na kuthibitishwa na TFF, haitatambuliwa”
Kaimu Rais wa TFF, Wallace Karia, akifunga hoja hiyo, amesema endapo kuna timu haitakidhi japo sharti moja kati ya hayo, basi mchezaji wake hatapewa leseni ya kucheza kwa msimu husika na kusisitiza “Wakati huu hatutaki siasa. Tusimamie kanuni hizi, hatutaki kuleta mchezo msimu huu.”
Kanuni ya 18 (1) ya ligi inasema: “Kila Klabu ina wajibu wa kuwawekea wachezaji wake bima ya matibabu na fidia kutokana na ajali michezoni. Klabu itakayokiuka kanuni hii itakuwa imepoteza sifa ya kuwa klabu ya Ligi Kuu, na usajili wa wachezaji wa timu yake hautathibitishwa na haitashiriki katika Ligi Kuu”.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment