Bulaya Ambwaga Tena Wasira Mahakamani

Mahakama ya Rufani imetupilia mbali rufaa iliyokatwa na wapiga kura wanne wa Jimbo la Bunda Mjini Mkoani Mwanza ya kupinga ushindi wa Mbunge, Esther Bulaya katika uchaguzi Mkuu wa Wabunge, Madiwani na Rais wa Tanzania ulifanyika Oktoba 25 mwaka 2015.

Wapiga kura hao ambao wanampigania aliyekuwa Waziri wa Chakula, Kilimo na Ushirika na mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Bunda Mjini, Stephen Wasira, wapo wanne ambao ni; Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Ascetic Malagila.

Uamuzi huo umetolewa jana na  Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Elizabeth Mkwizu ambapo alisema, upande wa walalamikaji uliwasilisha hoja 10 za kupinga ushindi wa Bulaya, lakini hoja hizo hazikuwa na mashiko, hivyo zinatupiliwa mbali.

Miongoni mwa hoja zao ni “Stephen Wassira, hakualikwa katika mchakato wa kujumlisha kura suala hili linaweza kuathiri matokeo ya uchaguzi kwa kushindwa kumtambua mgombea wala chama chake,”

Baada ya maamuzi hayo Mbunge huyo kupitia ukurasa wake wa twitter aliandika maneno machache ambayo alimshukuru Mungu kwa kitendo cha kushinda kesi hiyo dhidi ya wapiga kura hao.

"Wana bunda wameshinda tena na tena, asante Mungu", aliandika Bulaya.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment