BUNGE la taifa nchini Poland limepitisha muswaada unaolipa nguvu ya kuteua au kutengua viongozi wa mahakama kuu wakiwemo majaji wa juu, anaandika Catherine Kayombo.
Muswaada huo uliopitishwa na wabunge kutoka chama tawala cha PIS na washirika wao kwenye serikali ya mseto umesomwa kwa mara ya kwanza jana, Julai 19 na sasa kamati ya bunge inatazamiwa kuujadili kwa haraka.
Hatua hiyo imepata upinzani mkali kutoka kwa wananchi na wabunge wa upinzani na wamekosoa bunge kwa kudai linaingilia uhuru wa mahakama katika kusimamia haki za binadamu.
Usiku wa kuamkia leo, maelfu ya waandamanaji wa upinzani walikusanyika nje ya viwanja vya bunge wakipinga kupitishwa kwa sheria hiyo, hali iliyopelekea jingo la bug e kulindwa kwa vizuizi na walinzi wa serikali.
Kiongozi wa maandamano hayo, Pawel Kasprzak, amesema muswaada huo unamaanisha kwamba kanuni ya utenganishaji wa madaraka kwenye demokrasia ya Poland kwani hatua hii ni nia ya bunge kuweka udhibiti wake dhidi ya mahakama.
Kupitishwa kwa muswaada huo, kamisheni ya umoja wa Ulaya imetiwa wasiwasi na hatua ya serikali ya Poland kutaka kudhibiti mahakama kupitia bunge hivyo, imeitisha mkutano na kiongozi wa Poland rais Andrzej Duda.
0 comments :
Post a Comment