Kesi ya ‘Unga” dhidi ya Masogange yakwama tena Kisutu


Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeshindwa kuanza kusikiliza ushahidi
wa upande wa mashtaka katika kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili, Agnes Gerald maarufu Masogange baada ya wakili wa Serikali anayeiendesha kesi hiyo kuuguliwa na mwanaye.
Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 2 itakapoanza kusikiliza ushahidi huo.
Upande wa mashtaka ulipeleka mahakamani mashahidi wawili na mshtakiwa alikuwepo mahakamani.
Katika kesi hiyo, Masogange ambaye ni mrembo anayetumika kupamba video za wasanii, anadaiwa kati ya Februari 7 na 14, katika maeneo yasiyofahamika jijini Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya heroini (diacety/morpline) kinyume cha sheria.
Pia, anadaiwa kati ya tarehe hizo, alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam. Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment