kipa wa Serengeti Boys atua Yanga anadaka mpaka anakera.

Klabu ya Yanga ambayo siku ya kesho inatarajiwa kusafiri kwenda mjini Morogoro kwa kambi ya siku 10 kwa maandalizi ya Ligi Kuu Bara msimu huu imefanikiwa kunasa saini ya goli kipa wa Serengeti Boys, Ramadhani Kabwili.
Ramadhani Kabwili amesaini mkataba wa miaka mitano kuitumikia klabu ya Yanga ambayo imeweza kushinda Ligi Kuu Bara mara tatu mfululizo
“Ramadhani Kabwili, golikipa wa timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania (Serengeti Boys) amejiunga na Yanga SC kwa mkataba wa miaka mitano” ilisema taarifa Yanga
Kabwili ametua Jangwani baada ya klabu hiyo kuachana na makipa wake wawili Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’ ambao wamemaliza mikataba yao na kwenda katika klabu zingine, Kabwili anaungana Benno Kakolanya kipa pekee aliyekuwa amebaki Jagwani.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment