Mkuu wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amemuonesha Rais Magufuli kiwanda kingine ambacho amedai kuwa ni kikubwa kuliko viwanda vyote nchini kinachoweza kusaidia utekelezaji wa kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ya kujenga Tanzania ya viwanda.
Kiwanda hicho ni mchezo wa soka, ambapo Manara amesema endapo kitafanyiwa uwekezaji wa kutosha kitaweza kuzalisha ajira nyingi kuliko viwanda vyo ambavyo serikali ya awamu ya tano imepanga kuvijenga na kuviendeleza.
Manara amesema kwa kuwa Rais Magufuli ameonesha uwezo mkubwa katika masuala mengine ya kimaendeleo nchini ikiwemo kuongeza makusanyo ya mapato TRA, hawezi kushidwa kufanya mapinduzi katika sekta ya mpira wa miguu.
“TFF wanatakiwa waje na mpango wa kukiboresha na kukiunda kiwanda hiki sasa, maana mimi naona kama vile kiwanda hiki hakipo, serikali iwekeze kwenye football kuanzia chini. Kama Rais ameingia mahali, nchi nzima inatumia mashine za EFD, TRA makusanyo yameongezeka, ofisini kuna nidhamu ya kazi kwenye taasisi za umma, mambo yanakwenda, nakuhakikishia Rais akiingia hapa kwenye mpira, akaja kutuundia hiki kiwanda, ataacha legacy ambayo hajaacha Rais yeyote, na kisiasa itamsaidia sana katika uchaguzi wa 2020, kwa sababu hakuna kitu kinachopendwa zaidi katika nchi hii kama mpira” Amesema Manara.
0 comments :
Post a Comment