Manchester United yaichapa Real Madrid kwa penalti


Manchester United wameifunga Real Madrid kwa mikwaju ya penalti baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare ya goli 1-1.
Anthony Martial alitumia juhudi binafsi na kumtengenezea pande Jesse Lingard na kuandika goli la kwanza.
Casemiro aliisawazishia Madrid kwa njia ya penalti baada ya mlinzi mpya wa United Victor Lindelof kumuangusha Theo Hernandez katika eneo la hatari. Penalti saba kati ya kumi hazikuingia nyavuni.
Haukuwa usiku mzuri kwa Lindelof ambaye aliendeleza makosa yake na kukosa mkwaju wa penalti. United wameshinda michezo yote minne katika ziara nchini Marekani na watakutana na Barcelona katika fainali siku ya Jumatano.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment