TFDA Kanda ya Ziwa yateketeza tani 1.65 ya bidhaa chakula zisizokidhi viwango vya ubora


Mamlaka ya Chakula na Dawa ( TFDA ) Kanda ya Ziwa imeharibu bidhaa mbalimbali za chakula zisizokidhi viwango vya ubora na usalama vilivyokamatwa katika baadhi ya maduka ya jiji la Mwanza, huku ikiwatoa wasiwasi wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa juu ya madai ya kuwepo kwa mchele wa plastiki usiofaa kwa matumizi ya binadamu.
Bidhaa hizo zenye uzito wa tani 1.65 zikiwa na thamani ya karibu shilingi milioni 3 ni pamoja na chumvi aina ya kaysalt ambayo katika kifungashio imekutwa na maelekezo yaliyoandikwa ‘for sale in Kenya only’ na mafuta ya kula aina ya ufuta, ambazo zimeingizwa nchini bila kuzingatia taratibu za uingizaji bidhaa, kutokuwa na usajili kutoka TFDA, katika bidhaa hizo pia vimo vyakula vilivyokwisha muda wake wa matumizi pamoja na vyenye viwango duni.
Bidhaa hizo zimeharibiwa katika dampo la Buhongwa kutokana na uwezekano wa kuisababishia jamii madhara, kutofahamika kwa viwango vya ubora na usalama pamoja na kukinzana na matakwa ya sheria ya chakula, dawa na vipodozi namba 1 ya mwaka 2003, ambayo imeipa jukumu TFDA la kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa za chakula ili kulinda afya ya jamii.
Chanzo: ITV
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment