Kiongozi wa juu wa Tume ya Uchaguzi Huru na Mipaka (IEBC) amejiuzuru, akisema kuwa nchi yake haitaweza kuandaa uchaguzi huru na haki unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo.
Roselyn Akombe, amesema, IEBC imekuwa kwenye “kizungumkuti”, cha siasa nchini humo, na hivyo kushindwa kufikia makubaliano au uamuzi wowote.
Akiwa nchini Marekani anakofanyia kazi, ameiambia BBC kuwa, amekuwa na hofu na maisha yake alipokuwa nchini Kenya, baada ya kupokea vitisho vingi.
Juma lililopita, kiongozi wa upinzani, Raila Odinga alijitoa katika uchaguzi wa marudio wa urais unaotarajiwa kufanyika Oktoba 26.
Mahakama ya Juu nchini humo, ilifuta matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8, ambao ulimtangaza mshindi Rais wa sasa Uhuru Kenyatta baada ya kukiukwa kwa taratibu.
Katika taarifa yake, Akombe amesema amekuwa na ” wasiwasi juu ya uamuzi wake wa kuondoka IEBC (Independent Electoral and Boundaries Commission).
Na kuongeza ” Uamuzi wangu wa kuondoka IEBC unaweza kuwavunja moyo baadhi yenu, lakini siyo kwa kukosa kujaribu.
“Nimejaribu kwa kadri ya uwezo wangu kutokana na hali iliyopo. Kuna wakati unatakiwa kuondoka, hususan wakati pale maisha ya watu muhimu yanawekwa rehani. Tume hiyo imekuwa sehemu ya hali tete inayoendelea nchini humo.Tume hiyo imezingirwa.
“Tume hiyo kwa sasa haina uhakika wa kuendesha uchaguzi huru na haki Oktoba 26, 2017