Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe jana alizungumza na waandishi wa habari kueleza kuwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameinuka kitandani na ametoka ICU, lakini dokezo kwamba video inayomuonyesha akizungumza itatolewa leo, limeibua shauku ya kipekee na kuwa gumzo.
Taarifa ya video ya Lissu imeibua hamu ya watu kutaka kuiona, huku viongozi Lissu, ambaye ni mwanasheria mkuu wa Chadema, alishambuliwa kwa risasi zipatazo 32 akiwa ndani ya gari , nje ya makazi yake Area D mjini Dodoma,
ikiwa ni muda mfupi baada ya kutoka kikao cha asubuhi cha Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Hadi sasa, Jashi la Polisi halijatangaza kumshikilia mtu yeyote kwa kumuhusisha na shambulio hilo lililotokea Septemba 7 katika eneo la makazi ya viongozi ambayo yana ulinzi.
Alipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na usiku alisafirishwa kwenda Hospitali ya Nairobi, ambako alikuwa Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) hadi mwishoni mwa wiki iliopita