Klabu ya Simba itawakosa wachezaji wake John Bocco na Salim Mbonde kwenye mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Njombe Mji utakaopigwa Oktoba 21 mwaka huu, dimba la Uhuru Dar es Salaam.
Wachezaji hao ambao ni sehemu ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo wanakabiliwa na majeraha baada ya kuumia kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar uliopigwa Jumapili ya Oktoba 15 kwenye uwanja huo huo wa Uhuru Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara amesema Bocco ameumia kisigino cha mguu na Mbonde ameumia goti.
Katika mchezo huo, Bocco alitolewa nje mapema kabisa ikiwa ni dakika ya 14 ya mchezo wakati Mbonde akitolewa nje akiwa kwenye machela dakika ya 46
0 comments :
Post a Comment