Leo jumapili Agosti 17, 2017 Yanga wamecheza mchezo wa kirafiki na timu ya Polisi Tanzania.
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la uhuru jijini Dar majira ya saa kumi jioni ulimalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana.
Mchezo huo ulikosa msisimuko kutokana na watu wengi siku ya leo walikuwa wanafuatilia mchezo wa fainali ya CECAFA kati ya Kenya na Zanzibar.
Yanga imechezeha karibia wachezaji wote muhimu wa kikosi cha kwanza, Amis Tambwe alirejea uwajani leo baada ya kukaa nje kwa muda kadhaa kutoaka na majeraha yaliyokuwa yanamsumbua. Tshishimbi nae aliingia uwanjani kwenye mchezo wa leo akitokea majeruhi.
Licha ya hao,pia Yanga ilipata nafasi ya kumchezesha mchezaji mpya Yohana mkomola ambae alisajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili.
Haya ni maandalizi kwa Yanga kuelekea kwenye mchezo wao wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Reha Fc Disemba,24
0 comments :
Post a Comment